kigamboni community center (kcc)


 kcc ni kituo kinacholea watoto Yatima na watoto waishio kwenye mazingira magumu
nilipata bahati ya kutembelea,wengi wao ni vijana wadogo wanaohitaji msaada sio tu wa kifedha hata kimawazo pia










kusaidia watoto yatima sio lazima uwe na kitu kikubwa sana,kuna baadhi ya watoto yatima huvaa nguo moja tu mwaka mzima unaweza wapa hao watoto kama una nguo imekuruka badala
ya kuitupa shimon,Nenda kaitupe kwa hawa Watoto yatima ambao wapo vituo mbali mbali.Kwao itakuwa kama sikukuu na ni mpya tena sana.
Yatima wanahitaji sio tu hzo nguo wanahitaji pia
 chakula,
 sehemu ya kulala,
  elimu,
huduma za ziada kama Hospital n.k.

Ngoja niwape siri,Kusaidia watoto yatima ni sehem ya uwekezaji pia hakuna ajuaye kesho yake.Mungu hawezi kukuacha hata siku moja tena atakuheshim sana kuwa miongoni mwa watu wachache wenye upendo

ningependa kutafakari nawew hili neno la Mungu kutoka katika kitabu cha MATHAYO MTAKATIFU 25:34-40
"kisha mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume,Njoni,mliobarikiwa na Baba yangu,urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu
kwa maana nalikuwa na njaa mkanipa chakula,nalikuwa na kiu mkaninywesha,nalikuwa mgeni mkanikaribisha,nalikuwa uchi mkanivika nalikuwa mgonjwa mkaja kunitazama
Ndipo wenye haki watakapo mjibu wakisema  ,Bwana ni lini tulipokuona una njaa tukakulisha au kiu tukakunywesha?
Na mfalme atajibu ,akiwaambia,Amin ,nawaambia,kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo,mlinitendea mimi"

Ubarikiwe sana na Roho wa Mungu akuongoze baada ya kusoma makala hii, aufanye moyo wako kuwa mwepesi na kuona umuhimu wa kuwasaidia hawa ndugu zetu Yatima
sio lazima usaidie KCC vituo viko vingi sana Tanzania hata nje ya Tanzania.hicho ulicho nacho usione ni kidogo ni kikubwa sana kwa Wahitaji we peleka tu chochote na Mungu atafanya kitu juu ya Maisha yako

kwa KCC kituo kipo Kigamboni karibu na Mikadi beach au unaweza wasiliana na wakuu wa kituo kama utapata nafasi ya kuwatembelea

contact:0753 226 662
        0788 48 26 84
        0713 747 602 katibu kcc 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »